MAN CITY KUMJENGEA SANAMU KELVIN DE BRUYNE

 



Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, ametangaza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa klabu hiyo kuweka sanamu ya kiungo wake nyota, Kevin De Bruyne, nje ya uwanja wa Etihad. Hii ni kama ishara ya heshima kwa mchango mkubwa wa De Bruyne katika mafanikio ya timu hiyo kwa kipindi cha miaka 10.


De Bruyne ametangaza kuwa ataondoka klabuni mwishoni mwa msimu huu wa 2024/2025. Ameshacheza mechi zaidi ya 400, kufunga magoli 106 na kutoa pasi za mabao 174, akisaidia timu kushinda mataji 19, yakiwemo mataji 6 ya Ligi Kuu England na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Kama sanamu hiyo itathibitishwa, atajiunga na wachezaji wengine waliowahi kupewa heshima kama hiyo, akiwemo Vincent Kompany, David Silva na Sergio Agüero.


Source:Reuters 

 


Post a Comment

Previous Post Next Post