MO DEWJI ANAMZIDI UTAJIRI RONALDO


 Mjasiriamali na mfanyabiashara maarufu kutoka Tanzania, Mohamed Dewji (MO), ametajwa kuwa tajiri zaidi kuliko nyota wa soka duniani, Cristiano Ronaldo


Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni kutoka Forbes na vyanzo vingine vya kifedha, utajiri wa Mohamed Dewji unakadiriwa kufikia zaidi ya dola bilioni 1.5, wakati utajiri wa Ronaldo unakadiriwa kuwa takribani dola milioni 600.


Tofauti na Ronaldo ambaye amepata mafanikio kupitia soka na mikataba ya matangazo, MO amejijengea utajiri wake kupitia biashara mbalimbali za kilimo, viwanda, na huduma ambapo kampuni yake ya MeTL Group inaendesha shughuli katika zaidi ya nchi 8 barani Afrika.


Hii si tu ushindi kwa MO, bali ni ushindi kwa Tanzania Inaonyesha kuwa vijana wa Kiafrika wanaweza kufikia viwango vya juu zaidi duniani bila hata kutoka kwenye bara hili.


Post a Comment

Previous Post Next Post