![]() |
Kama kawaida naendelea kutoa maoni yangu, Kwanza kwa wasiojua maana ya IQ, IQ ni uwezo wa kufikiri kwa kina, kubuni, na kutatua matatizo kwa ubunifu. Hakuna data rasmi za vipimo vya IQ zao, haya ni maoni binafsi mimi @msumbufu_ nimetumia vigezo ninavyovijua mimi
🍁Professor Jay ; Mbali na muziki wake pia alihamia kwenye siasa, akionyesha uwezo wa kuyabena maswala ya kijamii na kuyawasilisha mjengoni kwa Lugha nyepesi
🍁Diamond Platnumz ; Ameonyesha ujanja mkubwa kwenye Biashara ya muziki, kuisimamisha lebo ya WCB na kujitengenezea fursa za kimataifa. Hiki ni kitu kinachohitaji uwezo mkubwa sana.
🍁Mrisho Mpoto; Mashairi yake yana tafakari kubwa ya kijamii na wana falsafa wanalisadifu hili, hii ni ishara tosha ya mtu mwenye akili kubwa ya uchambuzi.
🍁Ay (Ambwene Yesaya); Alikuwa mmoja wa waasisi wa muziki wa Bongo Fleva kwenye soko la kimataifa, akionyesha ubunifu na fikra za kimkakati.
NB: IQ si kipimo cha mafanikio ya msanii, lakini uwezo wa kubuni, kuelewa mwelekeo wa soko, na kuwasilisha ujumbe ni ishara za akili kubwa.
Unafikiri nani ana IQ kubwa na sijamtaja?
Post a Comment