BAJABER KUONDOKA SIMBA JANUARY


 ALIYEKUWA KOCHA WA SIMBA SC FADLU DAVIS ALIYEPENDEKEZA USAJILI WA BAJABER, SASA YARIPOTIWA KUWA ATAONDOKA JANUARI


Aliyekuwa kocha wa Simba SC, Fadlu Davis, ndiye aliyependekeza usajili wa kiungo Mohamed Bajaber kutoka Polisi FC ya Kenya, licha ya mchezaji huyo kuwa na jeraha wakati anasajiliwa. 


Ripoti zinaeleza kuwa Davis aliona uwezo wa Bajaber na kuamini kuwa ataweza kuwa msaada mkubwa kwa kikosi cha Simba mara baada ya kupona.


Hata hivyo, ingawa taarifa za hivi karibuni zilisema kuwa Bajaber ameanza mazoezi mepesi na kuonyesha dalili za kupona, leo hii kumeibuka habari mpya kutoka kwa chanzo cha karibu na klabu hiyo, kikidai kuwa Simba SC inapanga kuachana na mchezaji huyo ifikapo Januari mwakani.


Kwa mujibu wa chanzo hicho, nafasi ya Bajaber itachukuliwa na mchezaji Thabo Maponda kutoka klabu ya Gaborone United ya Botswana. 


Maponda anatajwa kuwa kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba na kupandisha mashambulizi, na Simba inadaiwa imekuwa ikimfuatilia kwa muda mrefu.


Uamuzi wa kuachana na Bajaber unaweza kuibua maswali kuhusu mchakato wa usajili wa klabu hiyo, hasa pale inaposajili wachezaji waliopo katika hali ya majeraha. 


Mashabiki na wachambuzi wa soka huenda wakataka majibu juu ya nani anawajibika kwa maamuzi hayo, hasa kama yatapelekea matumizi makubwa ya fedha pasipo faida ya moja kwa moja uwanjani.


Kwa sasa bado hakuna tamko rasmi kutoka klabu ya Simba SC kuhusiana na hatma ya Bajaber wala ujio wa Thabo Maponda, lakini kwa mujibu wa taarifa hizo, Januari inaweza kuwa kipindi cha mabadiliko makubwa ndani ya klabu hiyo yenye historia kubwa ya soka Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post