HUU UJUMBE WA SHAMSA KWA MAMA DANGOTE UMEZUA GUMZO


 ''Hakika huyu mama anastahili Pongezi nyingi sana.Huyu Diamond tunayemuona hapa bila uwepo wa mwanamke shujaa ambaye ni mama yake tusingemjua .Kuna mishale amepembana nayo ambayo tunaijua na tusiyoijua kwasababu ya mwanaye.Kuna vipengele vigumu Vya maumivu ukute alipambana navyo huyu mama lakini hakuwahi kukata tamaa na mwanaye.Bila huyu mama kumsapoti mwanaye na kuamini kwenye ndoto zake tusingekuwa na Diamond tunayejivunia AFRICA NZIMA.NYIE huyu mama amewakilisha single mothers wote kwamba lolote linawezekana kwa mwanao.Sisi tunamjua DIAMOND lakini anayemjua Nasibu ni huyu mama pekee. Namuongelea huyu mama aliyetuzalia kijana mpambanaji,kijana wa kitanzania kutoka familia ya kimasikini akaamua kuamini ndoto zake na leo hii anaitangaza TANZANIA yetu DUNIANI KOTE KUPITIA MZIKI WAKE🙌🏻🙌🏻.Hakika huyu mama anastahili TUZO Nyingi akiwa miongoni mwa wanawake MASHUJAA tulionao TZ. Upendo wa mama ni kinga kubwa kwa mwanaye.DIAMOND🙌🏻🙌🏻 diamondplatnumz Our hero mama_dangote

Wabongo utasikia unajipendekeza wakati ukweli wanauona😂😂'' Ameandika - Shamsa Ford

Post a Comment

Previous Post Next Post