IJUE SAFARI YA MAFANIKIO YA DIAMOND




  •  2009: Mwanzo wa Safari



Diamond aliachia wimbo wa “Nenda Kamwambie”.


Alirekodi wimbo huu kwa tabu, akikopa pesa kutoka kwa mama yake kwa ajili ya studio.


Hakukuwa na label, hakukuwa na meneja ni ndoto tu na kipaji.

Hapa ndipo jina lake lilipoanza kutajwa mitaani.


  • 2010: Mwaka wa Kuvunja Rekodi



Alitoa albamu yake ya kwanza “Kamwambie”, iliyobeba nyimbo kama Kamwambie, Nitarejea, na Mbagala.


Aliibuka mshindi wa Tuzo 3 za Muziki Tanzania (KTMA).


Kutoka msanii wa kawaida hadi kuwa gumzo la kitaifa.


Alihusishwa kimapenzi na Wema Sepetu Miss Tanzania 2006.


Mahusiano yao yakawa ya kwanza kumweka kwenye spotlight ya media za udaku.


  • 2011: Kujenga Jina



Diamond hakulala alitumbuiza kila kona ya Tanzania na Afrika Mashariki.


Aliendelea kuachia ngoma kama “Gongo La Mboto” akiwa na Mb Dogg na “Moyo Wangu”.


Alianza kutajwa kama sura mpya ya muziki wa Bongo Fleva.


Baada ya misukosuko mingi, uhusiano wake na Wema ukavunjika.

Aliandika nyimbo kama “Moyo Wangu” ambayo mashabiki walizihusisha na machungu ya mapenzi.

  • 2012: Kubadilika Kiubunifu



Alitoa nyimbo kama “Lala Salama” na “Mawazo”, akionyesha uwezo wa kubadilika na kubeba hisia tofauti.


Wakati huu alianza kujitangaza kama msanii wa kimataifa kwa kutumia video bora na mitindo ya kisasa.


Kipindi hiki alihusishwa na Mh. Jokate Mwegelo (Kidoti). Walionekana hadharani mara chache, lakini haikudumu.


  • 2013: Kushirikiana na Wakali



Wimbo wa “Number One” uliofanywa na producer wa Nigeria (Pheelz) ulimfungulia milango Afrika.


Hii ilifuatiwa na “Number One Remix” akiwa na Davido ushirikiano uliochochea jina lake kuvuma zaidi Nigeria na Afrika Magharibi.


Alijaribu mahusiano mengine ya kimya kimya, ikiwemo na mwanadada aitwaye Pennie. Mwishoni mwa mwaka, Diamond akarudi kwa Wema Sepetu kwa mara ya pili.

  • 2014: Diamond anakuwa Brand



Alianzisha lebo yake ya muziki WCB Wasafi. Huu ulikuwa mwanzo wa ndoto yake ya kuinua wasanii chipukizi kama Harmonize, Rayvanny, na wengine.


Aliendelea kutoa hits kama “Mdogo Mdogo”, “Nasema Nawe”.


Mahusiano na Wema yakaibuka tena lakini yakaanguka kwa mara ya mwisho.


Akatangaza rasmi kuwa yamekwisha.

Hapo ndipo Zari Hassan akaingia kwenye maisha yake…

  • 2015: Mapenzi na Umaarufu



Uhusiano wake na Zari Hassan uligeuka kuwa gumzo Afrika.

Walionekana kama “Power Couple” na walizaa watoto wawili.


Wimbo wa “Utanipenda” ulielezea hadithi ya mapenzi na maisha baada ya umaarufu.

  • 2016: Diamond Mataifa



Alishinda tuzo nyingi za kimataifa, akatumbuiza kwenye matamasha makubwa Afrika.


Wimbo wa “Kidogo” akiwa na P-Square ulionyesha kuwa Diamond haogopi kushirikiana na majina makubwa.


Wasafi ikawa empire.


Walizaa mtoto wa pili Nillan Dangote.

Wakati huo, Diamond alikuwa juu sana kitaifa na kimataifa.


Lakini drama ilianza kuingia…


  • 2017 hadi 2020: Kujiimarisha



Alifungua Wasafi FM, Wasafi TV, na kupeleka lebo yake kimataifa.


Hits kama “Jeje”, “Inama” (ft. Fally Ipupa), “Kanyaga”, na “Waah” (ft. Koffi Olomide) zilimuweka kwenye chati za Afrika kila mwaka.


Diamond akaingia kwenye orodha ya Forbes.


Diamond alizaa na aliyekua video vixen Hamisa Mobetto mtoto wao Dylan.Zari aligundua kupitia mitandao. Drama ikaanza, na media zikalipuka. Alikiri hadharani


2018 Zari alitangaza rasmi kuachana na Diamond kupitia post ya Instagram na Diamond akaachia “The Boy From Tandale” – albamu ya kimataifa.


  • 2021 – Sasa: Diamond ni Taasisi



Amekuwa msanii wa kwanza wa Afrika Mashariki kufikisha streams milioni mia+ kwenye platforms kama YouTube na Boomplay.


Ameshiriki Netflix series (Young, Famous & African), na amekuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wa Afrika.


Anapanga kuipeleka Wasafi duniani.

Post a Comment

Previous Post Next Post